Jana Fiston Mayele alifunga bao lake la 16 kwenye ligi kuu ya NBC akiwa na kikosi cha Yanga msimu huu
Mayele ameendelea kujichimbia juu kwenye msimamo wa wafungaji mabao kwenye ligi akiongoza kwa tofauti ya mabao sita dhidi ya wanaomfuatia katika nafasi ya pili
Nyota huyu wa Kimataifa kutoka DR Congo ana mechi tano za kuvunja rekodi yake ya mabao 16 aliyoweka msimu uliopita
Katika msimu huu Mayele amepachika mabao 29 katika mashindano yote, akifunga jumla ya mabao 49 katika mechi 73 za mashindano alizoitumikia Yanga tangu msimu uliopita
Katika msimu huu kuna nyakati Mayele alikuwa kwenye fomu ya kutisha akifunga mabao 17 katika mechi 17
Mayele ni mshambuliaji aliyekamilika, hahitaji kupigiwa debe kama wale wengine, takwimu zake zinazungumza!

ADVERTISE HERE