Yanga vs Kagera Sugar, hapatoshi Azam Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2023
Yanga vs Kagera Sugar, hapatoshi Azam Complex

Yanga inapiga hesabu za kutwaa ubingwa katika mechi tatu zinazofuata lakini Wananchi wanajua ugumu wa mechi hizo zilizoko mbele yao

Mechi tatu za Yanga zinazofuata ni dhidi ya Kagera Sugar, Simba na Singida Big Stars ambayo pia itakuwa na mechi nyingine dhidi ya Yanga kwenye nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Kesho Jumanne, April 11 Yanga inaanza mkakati wa kusaka alama tisa kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Mtanange huo wa kukata na shoka utapigwa uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku

Katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo ambao ni bahati tu ilikuwa upande wa Wananchi

Kagera Sugar walitawala na kutengeneza nafasi nyingi ambazo hawakuzitumia ikiwa ni pamoja na kukosa mkwaju wa penati

Hata hivyo wakati ule Kagera Sugar walikabiliana na Yanga ambayo ilitua Mwanza siku moja kabla ya mchezo wakitokea Tunisia ambako walifanikiwa kutinga makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Yanga iliunganisha moja kwa moja kutoka Tunisia mpaka Mwanza ambako mchezo huo ulipigwa baada ya ombi la kuahirishwa kugonga mwamba

Wakati huu Yanga inaikaribisha Kagera Sugar ikiwa katika nyakati nzuri. Ile 'fatigue' ambayo iliwakabiliwa wachezaji katika mchezo wa kwanza haipo

Hata hivyo mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar haujawahi kuwa mwepesi hasa wakati huu Kagera Sugar wakiwa wameimarika baada ya ujio wa Meckie Mexime

Kagera Sugar wamekuwa na muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo. Wao hawakuwa na mechi yoyote katika kipindi cha wiki tatu 

Baada ya kurejea kutoka Tunisia, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alifanya kikao na wachezaji wake kuwaeleza umuhimu wa mechi zinazofuata mbele yao

Nabi alisema wanakabiliwa na mechi ngumu lakini ndio nyakati ambazo wachezaji wanapaswa kuonyesha ubora wao kwa kuhakikisha wanashinda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’