Yanga inakabiliwa na mechi muhimu ya Ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambayo itapigwa uwanja wa Azam Complex, siku ya Jumanne April 11 2023
Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda mechi tatu zinazofuata ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo ukiwa ni ubingwa 29 katika historia
Baada ya Kagera Sugar, Yanga pia itahitaji kushinda mchezo unaofuata dhidi ya watani zao Simba ili kujihakikishia ubingwa mapema tu
Yanga inaweza kuanza shamrashamra za ubingwa baada ya mchezo dhidi ya Simba
Iwapo kama Simba watashindwa kupata ushindi huko Mbarali kwenye mchezo dhidi ya Ihefu Fc, kazi inaweza kuwa rahisi zaidi kwa Yanga kwani ushindi wa mechi mbili utawahakikishia kutangaza ubingwa wa 29 mapema tu kabla ya kupaa Nigeria kwenda kuikabili Rivers United
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema pasipo kujali matokeo ya wapinzani wao, ushindi katika mechi mbili zinazofuata utawaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 65 alama nane zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 57 huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 24