Mayele ni kipimo cha washambuliaji Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2023
Mayele ni kipimo cha washambuliaji Tanzania

Fiston Mayele tayari amethibitisha pasipo shaka kuwa yeye ni mshambuliaji bora kwa sasa ndani ya ligi kuu ya Tanzania Bara

Msimu huu ameweka kambani mabao 15 akiwa na nafasi ya kuongeza mabao yake katika mechi zilizobaki kuhitimisha msimu

Katika mashindano yote Mayele amefunga mabao 28. Amepachika mabao nane mechi za mtoano ligi ya mabingwa, amepachika mabao matatu kwenye kombe la Shirikisho na pia alifunga mabao mawili katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba mwanzoni mwa msimu

Mayele amefunga kila aina ya goli katika mabao hayo 28 aliyopachika. Ubora wake umempatia nafasi ya kuitwa kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo kwa mara ya kwanza katika mechi za kuwania kufuzu Afcon 2023 akipata nafasi ya kucheza katika mechi zote mbili

Kwa sasa Mayele ni kipimo cha mshambuliaji katika ligi ya Tanzania Bara, hivyo usishangae unaposikia anafananishwa na wengine

Sio dhambi kufananisha, lakini ukizungumzia ubora Mayele tayari amedhirisha ubora wake kwenye soka la Tanzania akifunga zaidi ya mabao 44 katika misimu yake miwili na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’