Winga Bernard Morrison amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa takribani miezi minne akisumbuliwa na majeraha
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimpa Morrison muda zaidi ya kufanya mazoezi wakati kikosi kikielekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao Yanga ilihitimisha hatua ya makundi kwa ushindi wa bao 1-0 na kujihakikishia kuongoza kundi D
Morrison ameandaliwa na sasa yuko tayari kutoa mchango wake katika mechi zinazofuata akianza na mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Morrison na winga kinda Denis Nkane wote wako fit na huenda wakawa na dakika zao katika mchezo dhidi ya Geita Gold siku ya Jumamosi
Β
ADVERTISE HERE