Bao alilofunga kiungo wa Yanga Mudathir Yahya katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe, limeshinda tuzo ya goli bora la hatua ya makundi katika kombe la Shirikisho
Mudathir alipachika bao hilo katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa akipokea pasi murua kutoka kwa Kennedy Musonda katika mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 3-1
Jumla ya kura 84, 166 zilipigwa katika ukurasa wa CAF wa Twitter, Mudathir akipata asilimia 70.5 ya kura zote
Wananchi wameupiga mwingiiii, wamehakikisha Mudathiri ameibuka mshindi...!
Choose your best #TotalEnergiesCAFCC group-stage goal now!
β TotalEnergies CAFCL - TotalEnergies CAFCC (@CAFCLCC) April 4, 2023
ADVERTISE HERE