Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Geita Gold
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, April 08 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam
Yanga ilirejea juzi kutoka Lubumbashi, DR Congo ambako walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe na kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kibabe kwa ushindi uliowaweka kileleni mwa kundi D
Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la FA na malengo yao ni kushinda taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo
Kama Yanga itapata ushindi siku ya Jumamosi, itacheza na Singida Big Stars katika hatua ya nusu fainali
ADVERTISE HERE