Baada ya Yanga kufanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwa vinara wa kundi D, Wananchi wameendelea kuchupa katika viwango vya ubora Shirikisho la soka barani Afrika (CAF)
Kwa mujibu wa msimamo uliotolewa baada ya kukamilika kwa mechi za makundi ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho, Yanga imechupa mpaka nafasi ya 20 kutoka nafasi ya 46
Msimu huu umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Yanga hata kuweza kuingia kwenye orodha ya timu 20 bora barani Afrika
Yanga ina nafasi ya kupanda zaidi kama itafanikiwa kutinga nusu fainali, fainali na watakusanya alama nyingi zaidi kama wataweza kuibuka mabingwa wa kombe la Shirikisho
Mkakati wa Yanga ni kutinga nusu fainali wakiwa na faida ya kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani kwenye mechi za robo fainali
