Baada ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kibabe kwa kuongoza kundi D, Yanga imerejea na sasa inaelekeza nguvu zake katika michuano ya kombe la FA
Jumamosi ya wiki hii Wananchi watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Geita Gold katika mchezo wa robo fainali katika michuano hiyo
Yanga wakiwa mabingwa watetezi, watakuwa wakisaka nafasi ya kutinga nusu fainali kwenda kuwavaa Singida BS ambao walitinga nusu fainali kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City
Ni mchezo mwingine mgumu dhidi ya Geita Gold ambao unapigwa palepale katika uwanja Azam Complex ambako mchezo wa ligi baina ya timu hizo ulipigwa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
ADVERTISE HERE