Kocha wa Township Rollers, Nikola Kavazovic amesema mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib ni msumbufu wamejipanga kumkabili vilivyo.
Yanga itashuka Uwanja wa Taifa kesho Jumanne saa 10 jioni kuwavaa Rollers katika mechi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi.
Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari, kocha Kavazovic alisema Yanga ni timu nzuri ila wapo tayari kuhakikisha wanapata matokeo yatakayowaweka vizuri kwa mchezo wa marudiano.
"Nimewaona Yanga katika mechi zao mbili za kimataifa ambazo walicheza hatua ya awali na St Luois ni timu nzuri ina wachezaji wazuri ambao wanaweza kucheza vizuri na kuipa matokeo," alisema Msebria huyo.
"Nimemuona Ibrahim Ajib wa Yanga mchezaji mzuri katika kumiliki mpira, kutengeneza nafasi za kufunga, na anavitu vingi vya kimpira ambavyo anaweza kuwa msumbufu kwetu, lakini kikosi changu kipo tayari kukabiliana na hilo," alisema Kavazovic.
Nahodha wa Township, Maano Pitshupo alisema "Si mara ya kwanza kwetu kuja hapa Tanzania kuna baadhi ya wachezaji ambao tulishakuja hapa na timu yetu ya Taifa Botswana kwa hiyo hatutakuwa wageni katika mazingira ya mechi yetu."
Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema wachezaji wa timu hiyo wanamorali ya kutosha kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Township Rollers.
Mkwasa alisema "tumefanya maandalizi ya kutosha kwani si timu ya kuibeza imeitoa moja ya timu kubwa Afrika katika hatua za awali jambo ambalo limeongeza umakini kwa upande wetu katika mechi hii ya nyumbani ambayo tunataka matokeo ya ushindi na si kingeni.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE