Mkwasa aita mashabiki uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2018
Mkwasa aita mashabiki uwanja wa Taifa
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kuipa sapoti Yanga itakapochuana na Township Rollers kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mkwasa amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika na wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

"Tunawaalika mashabiki wetu waje kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu yao kwenye mchezo huu wa kwanza tunaocheza nyumbani," amesema Mkwasa.

"Tumejiandaa kikamilifu, wachezaji wetu wanafahamu nini wanapaswa kufanya kesho. Hata hivyo tunahitaji sapoti kubwa ya mashabiki."

Mkwasa amesisitiza umuhimu wa kushinda mchezo huo ili kufuzu hatua ya makundi ambayo itawaingizia zaidi ya Bil 1 kutoka shirikisho la soka Afrika (Caf).

"Hii ni mechi kubwa na ya ushindani, mshindi anakwenda kwenye hatua za makundi. Kama mnavyofahamu hatua ya makundi wanasema ni 'money zone' ni eneo ambalo timu inapoingia kuna kuwa hakuna figisu za kutokuwa na pesa."

"Kufuzu hatua hii kutaleta mafanikio kwenye klabu kwa hiyo kila timu inapambana kufika pale ili kujaribu kupunguza japo gharama za maandalizi kwa sababu mashindano haya yanatumia gharama kubwa sana. Sisi tuna nia ya dhati kabisa kufanya vizuri na tumejipanga."

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho Jumanne kuanzia saa 10:30 jioni.

Viingilio;

VIP A - Tsh 20,000/-
VIP B na C - Tsh 10,000/-
Mzunguuko - Tsh 5,000/-
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’