Ushindi nyumbani ni muhimu - Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
5 Mar 2018
Ushindi nyumbani ni muhimu - Lwandamina
Kikosi cha Yanga kesho Jumanne kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya kwanza.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema tayari amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha wanashinda mchezo huo unaopigwa nyumbani.

“Maandalizi yameshakamilika muda mrefu, ukiwa na mtihani huwezi kujiandaa kwa siku moja kabla au wiki, nilishakiandaa kikosi changu muda, tunatakiwa tushinde ili tusonge mbele. Tunawahehimu wapinzani wetu, lakini tunataka ushindi nyumbani,” amefunguka Lwandamina.

Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kesho ikiwa kwenye kiwango bora baada ya kucheza michezo tisa bila kupoteza. Katika hiyo michezo, imeshinda michezo sita mfululizo ya ligi kuu ya Vodacom.

Yanga imedhamiria kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika. Kampeni hiyo ni lazima ianze na ushindi mnono nyumbani ili kurahisisha kazi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa March 17 nchini Botswana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6m ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →