Yanga Princess itaimarika - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Mar 2023
Yanga Princess itaimarika - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema wamefanya uwekezaji mkubwa katika Yanga Princess ili kuhakikisha timu hiyo inaimarika na kutwaa mataji

Arafat amesema mwenendo wa timu sio mzuri lakini anaamini wako katika njia sahihi keulekea mafanikio ya kweli

"Binafsi naridhishwa na maendeleo yao lakini nikiri kuna changamoto bado timu haijatulia kwa namna ambavyo tunataka wananchi, niseme jambo moja kuunda timu sio kitu cha usiku mmoja, sote tunajua jinsi tulivyounda hii timu yetu kubwa ambayo sasa tunajivunia"

"Mtaona jinsi tulivyoanza kwa kufanya usajili mkubwa kwa kuleta wachezaji wenye uzoefu na wanaochezea mataifa yao, lakini la pili tukalazimika kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kuleta kocha mwingine, hizi zote ni hatua za kujenga kitu kilichoimara, sasa tupo katika kuwachia makocha wafanye kazi zao lakini pia wachezaji kuzoea mazingira.

"Ukitazama ligi utaona hatujaachana sana na wanaongoza msimamo wa ligi, ukiniuliza nafasi ya ubingwa tutakubaliana kwamba bado ipo lakini tumewaachia makocha wetu kazi ya kuhakikisha klabu inafikia malengo yao wakati huu utawala nao tukitimiza wajibu wetu," alisema Arafat

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba Queens, kikosi cha Yanga Princess kinachonolewa na kocha Sebastian Nkoma kinashika nafasi ya nne kikiwa na alama 22 alama tano nyuma ya watani zao Simba Queens wanaoshika nafasi ya tatu

Fountain Gate Princess inaongoza ligi ikiwa na alama 29 ikifuatiwa na JKT Queens yenye alama 28 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’