Mkakati ni kuvuna alama tatu DR Congo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Mar 2023
Mkakati ni kuvuna alama tatu DR Congo

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga, Nasreddine Nabi amesema wanahitaji tena kupata ushindi dhidi ya TP Mazembe katika mchezo utakaopigwa Lubumbashi.

Yanga watakuwa wageni wa TP Mazembe April 02 kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku ikikumbuka ushindi wa 3-1 iliyoupata dhidi ya miamba hiyo ya DR Congo ilipocheza Uwanja wa Benjamin Mkapa mwezi uliopita.

Nabi amesema mchezo huo una umuhimu mkubwa sana kwa Yanga ambayo ina lengo la kumaliza kinara wa Kundi D na kuweka rekodi mpya katika historia ya Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na CAF.

Amesema kama kikosi chake kitaibuka na ushindi ugenini dhidi ya TP Mazembe kitajihakikishia kuwa kinara wa Kundi D, na kupata ahuweni ya kukutana na timu zitakazomaliza nafasi ya pili katika Kundi A, B na C.

"Sote tunafahamu kuwa kama tukimaliza nafasi ya kwanza kuna faida ya kukutana na timu za pili katika makundi mengine, lakini kama tukishindwa kupata nafasi hiyo tunaweza kuangukia kwa timu ambazo zimefanya vizuri kwenye hiyo michezo sita"

"Haitakuwa rahisi lakini mimi sio kocha rahisi wa kukata tamaa napenda kuishi kwa malengo nadhani kitu bora ni kujipanga na kucheza kwa hesabu sahihi, " alisema Nabi

Yanga inaongoza msimamo wa Kundi D ikiwa na alama 10 sawa na US Monastir ya Tunisia yenye tofauti ndogo ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku AS Real Bamako ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 05

TP Mazembe ambayo tayari imeshatupwa nje ya michuano hiyo inaburuza mkia ikiwa na alama 03, hivyo mchezo dhidi ya Young Africans utakuwa wa kukamilisha ratiba

Yanga inatarajiwa kuondoka Dar es salaam March 30 tayari kwa mtanange huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’