Yanga yarejea mazoezini kuiwinda TP Mazembe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2023
Yanga yarejea mazoezini kuiwinda TP Mazembe

Baada ya mapumziko ya siku tatu, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini leo kaunza maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe

Mchezo huo utapigwa April 02 huko Lubumbashi katika uwanja wa TP Mazembe

Utakuwa mchezo wa kukamilisha ratiba Yanga ikiwa tayari imefuzu robo fainali ya michuano hiyo lakini Wananchi wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza wakiwa vinara wa kundi

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji watashiriki mazoezi na kurejea makwao lakini March 27 wataingia kambini Avic Town kwa ajili ya kukamilisha maandalizi kabla ya safari ya DR Congo itakayokuwa March 30

Nyota wote ambao hawana majukumu ya timu za Taifa, wanashiriki program hizo za mazoezi. Wachezaji 12 wako katika majukumu ya timu za Taifa

Wachezaji hao ni walinda lango Djigui Diarra (Mali), Metacha Mnata (Tanzania)

Mabeki Kibwana Shomari, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakari Nondo Mwamnyeto (Tanzania)

Viungo ni Mudathir Yahya, Feisal Salum (Tanzania), Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso)

Washambuliaji ni Fiston Mayele (DR Congo) na Kennedy Musonda (Zambia)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’