Township Rollers lazima wakae uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2018
Township Rollers lazima wakae uwanja wa Taifa
Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa Jumanne March 06 kuikabili Township Rollers katika mchezo wa kwanza wa mtoano ligi ya mabingwa barani Afrika.

Township Rollers inatarajiwa kuwasili leo Jumapili baada ya jana kutwaa taji la Mascom Top 8 kwa kuichapa Orapa United mabao 4-2 kwenye mchezo wa fainali.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri baada ya kucheza michezo tisa mfululizo bila kufungwa, sita ikiwa ni ya ligi kuu ya Vodacom.

Aidha ushindi iliyopata hivi karibuni kusini mwa Tanzania kwa kuzifunga Majimaji 2-1 (kombe la FA) na Ndanda 2-1 (VPL), umeongeza morali ya wachezaji.

Yanga ilitokea Shelisheli ilikofuzu hatua hii ya michuano ya ligi ya mabingwa kabla ya kuzivaa Majimaji na Ndanda FC.

Yanga ina kikosi imara kinachoweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa keshokutwa hata bila kuwajumuisha wachezaji wake majeruhi wa muda mrefu Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambao imeelezwa wako kamili kurejea kikosini.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa haina presha zaidi ya kusaka ushindi kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi.

Licha ya wapinzani wao kuwa vinara kwenye ligi kuu ya Botswana, watakuwa na wakati mgumu kuikabili Yanga iliyo kwenye kiwango bora kabisa wakati huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’