Yanga Princess iko tayari kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' dhidi ya Simba Queens
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Uhuru, leo Jumatano March 22
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga Princess kusaka ushindi ili kuweka hai matumaini ya ubingwa msimu huu
Simba Queens inaongoza ligi ya Wanawake ikiwa na alama 26 wakati Yanga Princess inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 21
Ushindi kwa Yanga Princess utapunguza gap la pointi dhidi ya watani zao hao
Timu hizo ziligawana alama pointi katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ukimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
ADVERTISE HERE