Yanga na Nabi kuna malengo ya muda mrefu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Mar 2023
Yanga na Nabi kuna malengo ya muda mrefu

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema matunda yanayoonekana sasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanyika ndani ya klabu

Arafat amesema wamefanya usajili wa wachezaji bora na benchi la ufundi lililosheheni watu mahiri wakiongozwa na Profesa Nasreddine Nabi ambaye tetesi zimeanza juu ya kuhitajika kwake na vigogo wa soka barani Afrika hasa baada ya kuiongoza Yanga kutinga robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika

Arafat amesema klabu ina malengo ya muda mrefu hivyo haitakubali kocha wake aondoke kirahisi

"Kitu pekee ambacho kinatutofautisha na wapinzani wetu wengi ni kuwa na benchi la ufundi pana lenye wataalam bora"

"Nabi kuondoka linawezekana lakini haiwezi kuwa sasa, nadhani hata yeye anaamini yuko katika klabu ambayo hatua chache zijazo anaweza kuwa katika rekodi kubwa zaidi ya mafanikio," alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Bado tunamhitaji sana Nabi niwahakikishie mashabiki wetu kwamba kocha wao huyu na mwingine haitakuwa rahisi kwetu kuwaachia, tuna malengo makubwa na hii ni safari tu ya kufika huko"

"Tunafahamu hizi taarifa za sisi kuwa na kocha bora kama Nabi wengine ni ndoto zao, Yanga tuko katika mafanikio haya kutokana na kutumia nguvu kuwaweka wataalam wote bora kama hawa, utulivu wa namna hii klabu zingine hazina ndio maana wanayumba kila wakati"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’