Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ni mmoja wa wachezaji 27 waliojumishwa kwenye kikosi cha DR Congo kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 23
Hii ni mara ya kwanza kwa Mayele kujumuishwa kwenye kikosi kamili cha Congo DR
Amewahi kuitwa kwenye kikosi cha michuano ya CHAN kilichohusisha wachezaji wa ndani
Kikosi hicho kiliwahi kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania katika mchezo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 Mayele akifunga bao la DR Congo
Imekuwa sio rahisi kwa nyota wanaocheza ndani ya Afrika kupata nafasi ya kujumishwa timu ya Taifa ya DR Congo kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wa Taifa hilo wanaocheza barani Ulaya
Kwa nafasi ya ushambuliaji, Mayele ni mchezaji pekee anayecheza barani Afrika
Mayele ametimiza ndoto yake ya kuitumikia timu ya Taifa katika msimu ambao wengi wangeshangaa kama asingeitwa
Tangu atue Yanga Mayele amekuwa katika kiwango bora, ni mshambuliaji aliyekamilika!