Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amethibitisha kuwa kiungo Thabani Kamusoko atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Township Rollers katika mchezo wa ligi ya mabingwa keshokutwa.
Saleh amesema Kamusoko sasa yuko fiti kwa asilimia 100 baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi minne.
Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji waliokambini kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa March 06 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa kumi kamili jioni.
Mbali na Kamusoko, kinara wa mabao Obrey Chirwa naye huenda akarejea katika mchezo huo ingawa bado kuna wasiwasi kwa kuwa hakufanya mazoezi siku mbili zilizopita.
Licha ya kuanza mazoezi, mshambuliaji Donald Ngoma hatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Township Rollers keshokutwa lakini anaweza kuwa tayari kucheza kwenye mchezo wa marudiano siku 10 baadae kulingana na Meneja wa timu ya Yanga, Bw Saleh.
Beki Vicent Andrew na Amissi Tambwe hawatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi pia huku Yohana Nkomola, Juma Mahadhi na Abdallah Shaibu Γ’β¬ΕNinjaΓ’β¬Β nao wakiwa tayari kurejea baada ya kuanza mazoezi na kikosi cha Yanga.
Naye nahodha Nadir Haroub amerejea kikosini baada ya kumaliza msiba wa mwanawe uliotokea wiki mbili zilizopita

ADVERTISE HERE