Bacca alivyowazima Monastir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2023
Bacca alivyowazima Monastir

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya US Monastir ambao ulipigwa Tunisia, Yanga ilifungwa mabao 2-0 yote yakitokana na mipira ya kutenga

Jana Kocha Nasreddine Nabi akabadilisha walinzi wake wa wawili wa kati akiwaanzisha Bakari Nondo Mwamnyeto na Ibrahim Bacca badala ya Yannick Bangala na Dickson Job

Katika mechi za karibuni Nabi amemrejesha Bangala katika eneo la kiungo huku Job akikosekana katika mchezo wa jana nafasi yake ikichukuliwa na Bacca

Wachezaji wote walipambana kuhakikisha wanamuweka mlinda lango Djigui Diarra salama, lakini Bacca alifanya vyema kazi maalum iliyopelekea aanze mchezo wake wa kwanza katika michuano ya Shirikisho msimu huu

Bacca alikuwa kinara wa kuondoa mipira ya kichwa langoni kwani katika mipira saba aliyowania na wachezaji wa Monastir alishinda mitano

Haikushangaza kuona Monastir walikosa mbinu ya kuipenya ngome ya Yanga kwani silaha yao kubwa ni mipira ya kutenga ambayo wachezaji wa Yanga walijitahidi kutosababisha faulo karibu na lango au kona lakini hata ile waliyopiga iliokolewa kwa ustadi mkubwa na akina Baccca na Mwamnyeto

Nabi ameendelea kudhihirisha kazi yake nzuri katika benchi la ufundi akiimarisha viwango vya wachezaji wote

Sasa Yanga safu ya ulinzi wa kati iko katika mikono salama ya Mwamnyeto, Job na Bacca huku Mamadiu Doumbia akisubiri wakati wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
57m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’