Twendeni kwa Mkapa tukaisake robo fainali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Mar 2023
Twendeni kwa Mkapa tukaisake robo fainali

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga leo wana kazi moja tu pale uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir

Mchezo huu wa kundi D, ambao utapigwa saa 1 usiku, una umuhimu wa kipekee kwa Yanga kwani matokeo ya ushindi yatawahakikishia Wananchi kufuzu hatua ya robo fainali

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani leo kuwaongezea hamasa wachezaji wao katika mchezo ambao wanahitaji ushindi

Yanga imeandaa utaratibu wa aina yake ambapo msafara wa mashabiki utaanzia Jangwani majira ya saa 9 mchana kuelekea uwanjani

Kamwe amesema wingi wa mashabiki ni silaha muhimu kupata ushindi katika mchezo ambao hautakuwa rahisi

Monastir ndio vinara wa kundi D wakiwa na alama 10 wakifuatiwa na Yanga yenye alama saba

Monastir tayari wamefuzu hatua ya robo fainali lakini leo watakuwa wakisaka angalau alama moja ili kumaliza vinara wa kundi

Ushindi kwa Yanga utawahakikishia Wananchi kutinga robo fainali kwani watafikisha alama 10 ambazo haziwezi kufikiwa na TP Mazembe wala Real Bamako

Real Bamako na TP Mazembe zitachuana katika mchezo mwingine ambao utapigwa huko Mali

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi jana aliwaambia wanahabari kuwa wachezaji wake wako tayari, ari na morali yao iko juu

Hakuna jambo wanafikiria zaidi ya kushinda mchezo huo na kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-0 katika mchezo kwanza uliopigwa Tunisia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’