Baada ya kuanza msimu kwa kusuasua, winga wa Yanga Jesus Moloko kwa sasa yuko katika kiwango bora akiwa amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza
Katika kikosi cha kocha Nasreddine Nabi, Moloko ni miongoni mwa wachezaji wenye uhakika mkubwa wa kuanza mechi pale anapokuwa fit. Changamoto pekee ambayo imekuwa ikimuweka nje mara kwa mara ni majeraha
Moloko amesema kitu muhimu kwake ni kuisaidia Yanga kutimiza malengo hivyo anapopewa nafasi ya kucheza anapambana ili kuhakikisha anaendelea kupatiwa nafasi hiyo
"Kuna ushindani wa mkali wa namba, aliyepo benchi akipewa nafasi anapambana kwa kadiri kuisaidia timu, ndio maana sitaki kuichezea kabisa nafasi ninayopata nahitaji huduma yangu iwe muhimu kikosi cha kwanza"
"Ukifuatilia kwa ukaribu dakika nilizocheza sio nyingi msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita kutokana na majeraha ya mara kwa mara hilo halina afya kwangu ninapopata muda wa kucheza natakiwa kuutumia"
"Nitapambana kikosini hadi pale timu itakapofikia malengo nitapumzika nikiwa sina utimamu wa mwili au nimepata shida katika kujiandaa ama kwenye mchezo," alisema Moloko
Moloko amepachika mabao mawili katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Real Bamako na Geita Gold
Msimu huu kwenye ligi ametoa assist nne akiwa sawa na Joyce Lomalisa wakiwa ndio wachezaji wenye assist nyingi kwenye kikosi cha Yanga