Monastir waje tumalizane nao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Mar 2023
Monastir waje tumalizane nao

Kikosi cha Yanga kinaendekea kujifua Avic Town kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir ambao utapigwa Jumapili, March 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mechi muhimu kwa Yanga ikihitaji matokeo ya ushindi ili kuweza kutinga robo fainali ya michuano hiyo

Mashabiki na Wanachama wameendelea kuhamasishwa ili wajitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuwaongezea ari wachezaji wao katika mapambano ya kusaka ushindi

Umuhimu na ukubwa wa mechi hii pia inatosha kuwa hamasa kwa mashabiki kwani ni shauku ya kila Mwananchi kuona Yanga inatinga robo fainali

Huu unaweza kuwa msimu mzuri sana kwa Yanga katika michuano ya Shirikisho kama itafanikiwa kushinda siku ya Jumapili

Wananchi wakishajihakikishia kutinga robo fainali, watakuwa na nafasi ya kupambana kuwania uongozi wa kundi D

Faida ya timu inayomaliza kinara wa kundi ni kuanzia ugenini mechi ya kwanza ya robo fainali na kisha kucheza mechi ya pili nyumbani

Lakini pia mshindi wa kwanza wa kundi atacheza na mshindi wa pili wa kundi jingine katika hatua ya robo fainali

Mpangilio huu unatoa ahueni kwa timu kinara wa kundi na kuwa na nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema dhamira ya uongozi wake ni kuona Yanga inakuwa timu ya kwanza kuleta taji la michuano ya CAF nchini Tanzania

Hakuna jambo lisilowezekana, msimu huu Yanga inafanya vizuri, hivyo INAWEZEKANA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’