Droo ya robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imefanyika leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wamepangwa kuchuana na Geita Gold katika mchezo utakaopigwa jijini Dar es salaam
Ni mechi nyingine baina ya timu hizo itakwenda kupigwa palepale uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Siku chache zilizopita, Yanga iliichapa Geita Gold mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa hapo kunako uwanja wa Azam Complex
Katika droo hiyo pia imeshuhudia klabu ya Simba ikipangwa dhidi ya Ihefu Fc wakati Azam Fc wakipangwa kuchuana na Mtibwa Sugar huku Singida Big Stars wakiumana na Mbeya City
Aidha, TFF wameweka hadharani viwanja ambavyo mechi za nusu fainali na fainali zitapigwa
Nusu fainali ya kwanza itachezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona (Mtwara) na nusu fainali ya pili uwanja wa Liti (Singida) Fainali itachezwa katika uwanja wa Mkwakwani (Tanga).
Kama Yanga itavuka hatua ya robo fainali, kwenye nusu fainali itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Singida BS dhidi ya Mbeya City uwanja wa Liti
Mechi za robo fainali zitapigwa kati ya April 01-06 2023