Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate Princess kwa kufungwa bao 1-0 mkoani Dodoma, kikosi cha Yanga Princess leo Jumatano kitakuwa uwanjani mkoani Iringa kuikabili Mkwawa Queens
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga Princess kushinda ili kuendelea kuwa na matuamini katika mbio za ubingwa msimu huu
Kimahesabu bado Yanga Princess iko kwenye mbio za ubingwa kwani iko nyuma kwa tofauti ya alama tatu tu dhidi ya vinara Simba Queens wenye alama 23 sawa na Foutain Gate Princess
Kocha Mkuu wa Yanga Princess Sebastian Nkoma amesisitiza kuwa vijana wake bado wana nafasi katika mbio za ubingwa msimu huu
Uongozi wa Yanga umefanya uwekezaji mkubwa kwenye timu hiyo msimu huu kwa kuleta wachezaji wenye 'profile' kubwa

ADVERTISE HERE