Ngassa awakosha wengi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Mar 2018
Ngassa awakosha wengi
Mrisho Ngassa alin'gara sana wakati akiitumikia Yanga pengine kuliko wakati mwingine wowote wa maisha yake ya soka.

Mbali na Yanga, Ngassa amewahi kuzichezea Kagera Sugar, Azam FC, Simba, Free State Stars na Fanja ya Oman.

Baada ya kwenda kucheza soka Afrika Kusini, Oman na baadae kurejea nchini ambapo alijiunga na Mbeya City, kiwango cha winga huyo mwenye kasi kilionekana kutetereka.

Lakini tangu ajiunge Ndanda FC, Ngassa ameonekana kurejesha makali yake.

Katika mchezo wa juzi dhidi ya Yanga, Ngassa alitengeneza bao la kufutia machozi la Ndanda FC huku pia akichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo.

Ngassa amejaribu mara kadhaa kurejea Yanga, klabu ya ndoto yake bila mafanikio.

Nakumbuka wakati wa michuano ya Sportpesa baada ya msimu uliopita kumalizika, Ngassa alikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano hiyo kabla ya jina lake kukatwa dakika za mwisho.

Umri wake wa miaka 28 bado unamruhusu kuweza kurejea Yanga na kumaliza kazi ambayo mwenyewe anaamini hajaimaliza kama ataendeleza makali yake ya sasa.

Ngassa alijiunga Ndanda akitokea Mbeya City kwa mkataba wa muda mfupi unaomalizika mwishoni mwa msimu, hivyo atakuwa mchezaji huru mwezi Juni 2018.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’