Mabingwa watetezi ligi kuu ya NBC, Yanga jioni ya leo majira ya saa 12 watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kumenyana na Geita Gold katika mchezo wa ligi raundi ya 24
Wakati msimu ukielekea ukingoni, hesabu za Yanga ni kushinda mechi nne zinazofuata ili kutetea ubingwa wao kwa msimu wa pili mfululizo
Ushindi dhidi ya Geita Gold siku ya leo utaisogeza Yanga karibu na kutimiza malengo
Hata hivyo mechi kati ya Yanga dhidi ya Geita Gold haijawahi kuwa nyepesi. Yanga imefanikiwa kuibua na ushind wa bao 1-0 katika mechi zote za ligi walizikutana na Geita Gold tangu msimu uliopita
Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi ya kushinda mechi 10 mfululizo kwenye ligi
Tangu wapoteze mchezo dhidi ya Ihefu Fc, Wananchi wameshinda kila mechi waliyocheza kwenye ligi wakikusanya alama 30 ambazo zimewaimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 62 alama tano mbele ya Simba yenye alama 57
Mtanange utapigwa kuanzia saa 12:15 jioni