Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda amesema wachezaji wako tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo huo wa raundi ya nne kundi C, utapigwa kuanzia saa 1 usiku Yanga ikihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa kundi hilo
Baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo uliopita nyumbani dhidi ya TP Mazembe, Musonda ameahidi kuendeleza pale alipoishia
"Sisi tuko tayari, tunawaita mashabiki waje kwa wingi washuhudie historia ikiandikwa," alisema Musonda
Musonda alifunga bao moja katika mchezo dhidi ya TP Mazembe huku akitengeneza bao la pili lililofungwa na Mudathir Yahya
Bila shaka kesho atakuwa sehemu ya kikosi kitachoshuka dimba la Mkapa kumenyana Real Bamako katika mchezo ambao Yanga inahitaji kushinda