Baada ya Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki kuitwa timu za Taifa kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023, mlinda lango Djigui Diarra na mshambuliaji Kennedy Musonda nao wameitwa timu za Taifa
Diarra amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kwa ajili ya mechi dhidi ya Gambia wakati Musonda amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia kwa ajili ya mechi dhidi ya Lesotho
Aidha Mganda Khalid Aucho anatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Uganda ambacho kitacheza na Tanzania

Mechi za kusaka tiketi ya Afcon 2023 zitapigwa baada ya mechi za mzunguuko wa tano michuano ya CAF ambazo zitapigwa March 17-19
Nyota wengine wa ndani wanatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho kitacheza na Uganda