Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe leo aliongoza mazoezi ya vikundi vya ushangiliaji yaliyofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Jumatano, March 08 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Kutakuwa na nyuki wa njano na nyuki wa kijani siku hiyo ambao kazi yao itakuwa kuchangamsha majukwaa kwa ushangiliaji na kuwazomea wapinzani kwa muda wote wa mchezo
Yanga imejipanga, Real Bamako watakutana na mazingira ambayo hawakuwahi kukutana nayo kabla!




ADVERTISE HERE