Timu ya Yanga Princess imejipanga kuvuna pointi tatu muhimu katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara dhidi ya Fountain Gate Princess utakaochezwa Machi 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini, Dodoma
Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma, amesema wachezaji wake wanaendelea vyema kuelekea mchezo huo ambao wanaamini utakuwa na ushindani
Nkoma amesema wachezaji wake wameahidi kupambana ili kuvuna pointi tatu na kujiimarisha kwenye mbio za kuwania ubingwa wa msimu huu.
"Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu, tutahakikisha tunakwenda kubeba pointi tatu za ugenini, tunajua mechi haitakuwa rahisi," alisema Nkoma.
Aliongeza makosa ambayo aliyaona katika michezo iliyopita ya mzunguko wa kwanza ameyafanyia kazi kwa malengo ya kutojirudia katika michezo inayofuata.
Alisema wachezaji waliokuwa majeruhi wanaendelea vizuri na kikosi chake kitaondoka Dar es Salaam Jumatatu kuelekea Dodoma.
"Jumatatu tunatarajia kuanza safari ya kuelekea Dodoma tukiwa na matumaini makubwa ya kushinda, tunaomba mashabiki wetu waendelee kutuamini. Ligi ya msimu huu ni ngumu zaidi, timu zote zimeimarika, hatuna mechi rahisi"