Yanga imeongeza mtaalam mwingine katika benchi la ufundi ambaye jukumu lake litakuwa kuzisoma timu pinzani katika mashindano mbalimbali
Khalil Ben Youssef tayari ameanza majukumu yake katika nafasi ya 'Video Analyst'
Khalil raia wa Tunisia mwenye leseni B ya CAF amewahi kuzitumikia klabu za Al Ahly Tripol, Club Africain na Esperance ya Tunisia
Mahitaji ya soka la kisasa yanawahitaji wataaam kama Khalil ambao wanaweza kufanya uchambuzi yakinifu kwa timu pinzani na hivyo kulirahisishia kazi benchi la ufundi katika mbinu

ADVERTISE HERE