Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam leo wakitokea nchini Mali ambako walifanikiwa kupata alama moja kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Fiston Mayele ni mfungaji wa bao la Yanga ambalo liliwahakikishia kitita cha Tsh Milioni 5 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan
Yanga sasa imevuna Tsh Milioni 20 za Mama ikiwa imefunga mabao manne hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika

ADVERTISE HERE