Mafanikio hayaji kwa bahati mbaya - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2023
Mafanikio hayaji kwa bahati mbaya - Manara

Msemaji wa zamani wa klabu ya Yanga Haji Manara ambaye bado yuko ndani ya kifungo cha TFF, amesema mafanikio ambayo Yanga inapata sasa hayakutokea kwa bahati mbaya

Manara amesema uwekezaji wa kifedha na rasilimali watu ni moja ya sababu ya kuiweka Yanga hapo ilipo

"Idadi ya Watumishi wa Yanga ni kubwa mara mbili ya idadi ya Watumishi wa klabu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania"

"Kiufupi Yanga imetoa ajira katika kila idara inayotakiwa katika kuendesha football, ikiwa na Wafanyakazi wa kutosha wenye mikataba sahihi"

"Ukiona mambo yanaenda basi nyuma yake kuna hilo kundi ambalo ndio linalosimamia kazi za kila siku za Taasisi hiyo kubwa zaidi ya kispoti nchini"

"Alama nane juu zaidi katika msimamo wa ligi, nafasi ya pili kwenye msimamo wa CAF, Bingwa Mtetezi wa Mataji yote nchini na yale yote yanayofanyika nje ya uwanja, yanapaswa kuwe na Management imara na iliyoshiba kama hii," aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’