Mazungumzo ya mkataba mpya baina ya mshambuliaji Ibrahim Ajib na uongozi wa Simba yamevunjika baada ya pande mbili kushindwa kufikia mwafaka, imefahamika.
Uongozi wa Simba umeamua kumuacha mchezaji huyo akajiunge na timu yoyote anayotaka wakidai hana 'Spirit' ya kuendelea kuitumikia Simba.
Kulingana na mtandao wa ShaffihDauda, kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe na mtandao huo amethibitisha uamuzi wa Simba kuachana na Ajib.
"Tumejaribu kukaa na Ajib kwa ajili ya mazungumzo ili andelee kubaki Simba lakini mchezaji huyo hakuonekana kuwa tayari kubaki Msimbazi kutokana na kiwango cha pesa alichokua akikihitaji," alisema kiongozi huyo.
“Tumemwacha aende anakotaka kwenda kwa sababu hana ‘spirit’ tunayoihitaji sisi, acha aende tu sisi mbele kwa mbele.â€
Sasa ni dhahiri mchezaji huyo anaweza kujiunga na Yanga ambayo imekuwa ikimuwania kwa muda mrefu.
Licha ya Singida United kuhusishwa na mchezaji huyo, uwezekano wa kujiunga katika timu hiyo ni mdogo kwa kuwa mwenyewe Ajib anataka kucheza timu inayoshiriki michuano ya Kimataifa ili aweze kujiuza kimataifa atimize ndoto zake za kwenda kucheza soka la kulipwa nje.

ADVERTISE HERE