Jana kiungo Khalid Aucho alishindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Real Bamako akilazimika kutoka kwenye dakika ya 32 baada ya kufanyiwa madhambi
Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa Aucho hakupata majeraha makubwa hivyo atakuwa tayari kutumika katika michezo inayofuata
Taarifa iliyotolewa na Yanga imebainisha kuwa Aucho alipata michubuko chini ya goti iliyomfanya asikie maumivu makali
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Aucho amewashukuru wote walimtakia kheri kufuatia majeraha hayo huku akibainisha anaendelea vizuri
Hii ni habari njema kwa Wananchi kuelekea mechi mbili muhimu nyumbani kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako na US Monastir
ADVERTISE HERE