Kikosi cha Yanga leo kitakamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa raundi ya tatu hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili, Februari 26, stade du 26 Mars saa 1 usiku kwa saa za Tanzania, Mali itakuwa saa 10 jioni
Jana Yanga ilifanya mazoezi ya kwanza katika Mji wa Bamako ambako ndiko wenyeji wao walipo
Yanga ina jambo lake kwenye michuano ya kombe la Shirikisho msimu huu, kuisaka robo fainali
Ushindi ndio kipaumbele lakini ikiwa tofauti hata alama moja itakuwa na faida









ADVERTISE HERE