Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kuendelea kuiombea timu yao kuelekea mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Jumapili, Februari 26 huko Mali
Kikosi cha Yanga kiliwasili Mali jana majira ya saa 9 mchana (saa 12 Tanzania) na wachezaji kupata muda wa kupumzika kabla ya kufanya mazoezi ya 'recovery' kuondoa uchovu wa safari ya takribani masaa 10
"Timu imewasili salama Mali, tumeweka kambi katika hotel yenye hadhi ya nyota tano, Yamey, timu itakuwa na session moja ya mazoezi ya recovery kuondoa uchovu wa safari."
"Tutakuwa na session moja ya mazoezi Ijumaa saa 10 jioni na tutakuwa na awamu nyingine ya mazoezi Jumamosi saa 10 jioni muda ambao mchezo utapigwa"
"Tunawaomba mashabiki na wanachama wetu waendelee kutuombea ili tuweze kupata ushindi siku ya Jumapili," alisema Kamwe
Kamwe amesema pamoja na hali ya hewa ya joto katika Mji wa Bamako, lakini sio la kuwasumbua wachezaji kwani tofauti yake na jijini Dar es salaam sio kubwa sana
Joto linakuwa kali sana majira ya jioni saa 10 muda mabao mchezo huo utapigwa. Kiwango cha juu hufikia nyuzi joto 38