Juzi Yanga ilivuna jumla ya Tsh Milioni 33 zikiwa ni ahadi kutoka kwa viongozi mbalimbali baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika
Milioni 15 zikitoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Mama Samia Suluhu Hassan ambaye alitoa ahadi ya kununua kila goli kwa Tsh Milioni 5
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema ahadi hiyo haikuishia katika mechi iliyopita, itaendelea hata kwa mechi zilizobaki katika michuano ya ligi ya mabingwa ambayo Simba inashiriki na kombe la Shirikisho ambayo Yanga inashiriki
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Februari 26 huko Mali
Nafasi nyingine kwa wachezaji wa Yanga kula pesa ya Mama!


ADVERTISE HERE