Baada ya mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alimdaka winga Felippe Kinzumbi na kufanya mazungumzo nae ya muda mfupi
Kinzumbi aliisumbua sana ngome ya Yanga, unaweza kusema alikuwa nyota wa mchezo kwa upande wa kikosi cha TP Mazembe
Yanga inajipanga kuimarisha eneo lake la washambuliaji wa pembeni, Kinzumbi anaweza kuwa ingizo sahihi kwenye kikosi cha Nabi
Habari njema ni kuwa mkataba wa Kinzumbi na TP Mazembe unamalizika mwezi Juni 2023 yaani mwishoni mwa msimu huu
Kinzumbi anaitumikia TP Mazembe kwa mkopo akitokea JS Groupe Bazano. Walimsajili Machi 08 2020 kwa mkataba wa mkopo wa miaka mitatu
Mwanzoni mwa msimu huu Kinzumbi alikuwa na mgogoro na TP Mazembe akipinga jaribio la klabu hiyo kutaka kuongeza muda wa mkataba wake pasipo makubaliano
Mazembe walitaka kuandikisha mkataba wa miaka mitano kwenye mfumo wa FIFA pasipo kumshirikisha