Shamra shamra za ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe zimehitimishwa rasmi sasa Yanga ikielekeza nguvu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini leo Jumanne na moja kwa moja kuingia kambini kukamilisha maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa Jumatano, Februari 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ina mechi nane za kutetea ubingwa ambapo Wananchi wanahitaji kushinda mechi sita zinazofuata ili kukamilisha malengo
Baada ya mchezo dhidi ya KMC, Yanga itakwea pipa kuelekea Mali tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako ambao utapipgwa Jumapili, Februari 26
ADVERTISE HERE