Mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa jana walikuwa chachu kwa timu yao kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe na kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya robo fainali
Mashabiki wa Yanga jana 'hawakuzubaa' kama ilivyokuwa wa wenzao wa Simba juzi
Kulikuwa na 'vibe' ya aina yake kwa muda mwingi wa mchezo, hivi ndivyo mechi za nyumbani zinapaswa kuwa
Bila shaka mchezo utakaofuata nyumbani dhidi ya Real Bamako uwanja utafurika kwa asilimia 100
Lakini pia wachezaji wa Yanga jana hawakuwaangusha mashabiki wao, wametimiza kile walichoahidi
Ari na morali ya timu ilikuwa juu sana wachezaji walijitoa kwa asilimia 100 kuipambania timu
Kuna wakati kwenye kipindi cha kwanza Tp Mazembe walipoteana kabisa kwani Yanga iliwafunika kila eneo
Kocha wa TP Mazembe Mihayo Kazembe alilazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili ndani ya dakika 30 za kwanza, kwa sababu vijana wake walizidiwa hasa eneo la kiungo
Kennedy Musonda jana aliwafunga midomo wale wachambuzi wa michongo na wakosoaji wake
Amedhihirisha ni mchezaji wa mechi kubwa, kafunga bao na katoa 'assist' ya bao la Mudathir Yahya
Kocha Nasreddine Nabi huyu ni halali kuitwa Profesa kwani ni mtaalam wa kusoma wapinzani na kutengeneza timu yake kwa kufuata mahitaji ya mchezo
Inakupasa uwe jasiri sana kumuweka nje mchezaji kama Stephane Aziz Ki na nafasi yake kuanza na Mudathir ambaye wengi tunafahamu ni kiungo mkabaji
Ilikuwa sapraiz kwa Mazembe kwani hawakumfahamu vyema Mudathir na ndiye mchezaji aliyewavuruga sana kwenye kipindi cha kwanza
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto amerejea katika ubora wake, Nabi sasa hana sababu ya kumtumia Yannick Bangala katika eneo la safu ya ulinzi
"Kapten Beka" anatosha pale nyuma, akishirikiana vyema na kina Dickson Job, Ibrahim Bacca na Mamadou Doumbia ambaye bado Nabi anamuandaa kabla ya kumuingiza kikosini
Djuma Shabani katika ubora wake jana, Lomalisa, Bangala, Moloko, Mayele na Kisinda walihakikisha ndugu zao kutoka DR Congo hawatoki salama
Khalid Aucho ni yuleyule, kiwango atakachokupa katika mchezo dhidi ya Dar City ni kilekile amekupa kwenye mechi kubwa dhidi ya TP Mazembe
Mabingwa mara tano Afrika, TP Mazembe wamekufa kifo cha mende hapo kwa Mkapa, halafu anatokea mtu anakwambia Yanga hii ni dhaifu
Msimu huu kuna maajabu mkubwa yanaenda kutokea Jangwani...!