Lwandamina bado hajamaliza kazi iliyomleta Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2018
Lwandamina bado hajamaliza kazi iliyomleta Yanga
Tetesi zinazomuhusu kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kutakiwa na timu yake ya zamani ZESCO zimeshika kasi wiki hii ambapo huko Zambia taarifa hii imeripotiwa sana na vyombo vya habari.

Hata hivyo Lwandamina bado ana mkataba na Yanga unaomalizika Juni 2018 kulingana na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa.

Hivyo hawezi kuondoka kirahisi rahisi tu.

Kingine ni kwamba Lwandamina aliletwa Yanga kwa kazi moja kubwa, nayo ni kuiinua Yanga katika michuano ya Kimataifa, kazi ambayo bado hajaimaliza.

Rekodi za kocha huyu wakati alipokuwa ZESCO zilimfanya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji kumleta nchini

Lengo lake kubwa ilikuwa kuhakikisha ashirikiane na aliyekuwa kocha wakati huo Hans van Pluijm kuipeleka Yanga kwenye level za kimataifa.

Na ndio maana kikaanzishwa cheo cha Mkurugenzi wa Ufundi ambacho alikabidhiwa Pluijm.

Hata hivyo 'majanga' aliyopata Manji yalivuruga mipango yote hiyo.

Licha ya changamoto nyingi baada ya kuondoka Manji, Lwandamina aliamua kubaki Yanga ili kutimiza kile kilichomleta.

Wakati fulani ilielezwa kuwa Yanga ilikuwa na changamoto ya kulipa mishahara ya wachezaji wake, Lwandamina aliridhia awe wa mwisho kulipwa mshahara kwa maana mshahara wake walipwe wachezaji kwanza.

Licha ya mazingira magumu, Lwandamina amefanikiwa kutengeneza timu isiyotegemea mchezaji mmoja mmoja.

Leo hii Yanga inaweza kushuka dimbani na kuibuka na ushindi bila ya kuwa na mchezaji hata mmoja mwenye jina kikosini.

Lwandamina pamoja na benchi lake la ufundi wameshafanya kazi kubwa sana kuifika Yanga mahali ilipo leo hivyo naamini ataendelea kuwepo ili atimize malengo yake.

Nayo ni kuhakikisha Yanga inatinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwaka huu.

Ni dakika 180 tu zilizobaki kuiwezesha Yanga kutinga hatua hiyo kwa mara ya pili katika Historia yake.

Mwaka 1998 Yanga ilicheza makundi ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’