Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amebainisha kuwa wachezaji wako tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ukizungumzia wachezaji waliobeba matumaini ya Yanga katika mchezo huo Aziz Ki ni mmoja wao
"Mawazo ya kishujaa, haturudi nyuma na kamwe hatukati tamaa," Aziz Ki aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Tangu kikosi cha Yanga kiliporejea kutoka Tunisia ambako walipoteza mchezo dhidi ya US Monastir kwa kufungwa mabao 2-0, Yanga imejichimbia kambini Avic Town kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe
Aziz Ki pamoja na wenzake wanafahamu, mashabiki wa Yanga wanahitaji furaha katika uwanja wao wa nyumbani hapo kesho
Wananchi wamechoka kutoka dimba la Mkapa wakiwa wanyonge