Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua tiketi na waingine kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe
Manara amesema mashabiki wa Yanga hawana sababu ya kuwa wanyonge kuelekea mchezo huo kwani wana timu yenye wachezaji bora ambao wanaweza kupata ushindi dhidi ya Mazembe
"Kwanini tunakuwa wanyonge Wananchi?, kwanini tunashindwa kuwaambia watu juu ya ubora wa wachezaji wetu?"
"Tutumie ubora wa wachezaji wetu tulionao kuwajenga mashabiki wetu kwamba Mazembe hatoboi na twendeni uwanjani kwa wingi kwani silaha kubwa katika mechi kama hizi ni kujiamini," alisema Manara
TP Mazembe iliwasili nchini jana jioni tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Jumapili saa 1 usiku Yanga ikihitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano hiyo