Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan kutoa Tsh Milioni 5 kwa kila goli litakalofungwe kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe, ni amri kwao
Kamwe amesema wamejiandaa na watapambana ili kupata ushindi katika mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumapili, Februari 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kamwe amesema Yanga itatumia silaha zote walizonazo ili kushinda mchezo huo
"Hii ahadi ya Mh Rais Dk Samia Suluhu kwetu ni kama amri hivyo tunapaswa kushinda mchezo huo na tutatumia silaha zetu zote kufanikisha hilo," alisema Kamwe
Aidha Kamwe amesema kwa wale wenye maswali kuhusu kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' waje uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili kupata majibu yao
"Feisal ni mchezaji wa Yanga, wale wenye maswali kuhusu mchezaji wetu waje uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili"