Winga wa Yanga Denis Nkane ameendelea kuimarika baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki sita akiuguza majeraha
Nkane tayari ameanza mazoezi na anatarajiwa kuungana na wenzake wanaorejea leo kutoka Tunisia kuelekea maandalizi ya mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa siku ya Jumapili
Katika mechi za hivi karibu mawinga tegemeo Jesus Moloko na Tuisila Kisinda hawakuwa katika ubora wao kwa asilimia 100 na kupelekea baadhi ya mashabiki kutamani kuona kinda huyu akitumika
Hata hivyo huenda asiwe tayari kuwakabili TP Mazembe lakini anaweza kuwepo kwenye mchezo utakaofuata dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Februari 26 huko Mali
Mbali na Nkane, wachezaji wengine ambao wanaweza kutumika katika eneo la winga ni Dickson Ambundo, Farid Mussa na Bernard Morrison ambaye ni majeruhi
Baadhi ya mechi Nabi aliwatumia Clement Mzize na Kennedy Musonda katika eneo la winga
Huenda mabadiliko kama hayo yakashuhudiwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe