Tunapozungumzia kikosi cha historia ni kile kilichoichapa Club Africain bao 1-0 na kutinga hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Ni kikosi cha historia kwa sababu kiliifanya Yanga kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kupata ushindi katika ardhi ya Tunisia
Lakini pia kikosi kile kilijijengea heshima kwa kuibuka na ushindi katika mchezo ambao Yanga haikupewa kabisa nafasi na wengi hapa nchini
Leo tena katika uwanja uleule, Olympique Hammadi Agrebi Yanga inacheza na US Monastir mchezo wa kwanza wa hatua makundi Shirikisho
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ana nafasi ya kutumia kikosi kilekile leo isipokuwa wachezaji wawili tu ambao wamekosekana
Winga Bernard Morrison ni majeruhi wakati Feisal Salum bado hatma yake haijafahamika tangu alipojiengua kikosini
Nabi anayo maingizo mapya katika kikosi chake, nyota wanne Metacha Mnata, Mamadou Doumbia, Mudathir Yahya, Kennedy Musonda huku Djuma Shabani aliyekuwa majeruhi katika mchezo huo nae akirejea
Katika mchezo uliopigwa Novemba 09 2022, Nabi alianza na Diarra langoni wakati walinzi wa pembeni walikuwa Joyce Lomalisa na Kibwana Shomari
Walinzi wa kati walikuwa Dickson Job na Yannick Bangala wakati viungo walikuwa Khalid Aucho na Salum Abubakar 'Sure Boy'
Feisal Salum na Fiston Mayele walianza katika eneo la ushambuliaji wakati Morrison na Jesus Moloko walianza eneo la winga
Baadae Aucho alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Stephane Aziz Ki ambaye pasipo shaka leo ataanza mbele na Mayele
Katika mchezo huo Farid Mussa pia aliingia kuchukua nafasi ya Moloko
Aziz Ki, Farid, Sure Boy na Mayele ndio wlaihusika katika upatikanaji wa bao la Yanga
Nabi anarejea Tunisia akiwa na jeshi lilelile isipokuwa wachezaji wawili tu huku wengine watano wakiongezeka katika kikosi chake