Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo majira ya saa 1 usiku watashuka Stade Olympique Hammadi Agrebi kuwakabili wenyeji wao US Monastir katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika
Baada ya siku nne za maandalizi huko Tunisia, Yanga leo inakwenda kusaka alama tatu muhimu katika mkakati wao wa kucheza robo fainali ya michuano hiyo msimu huu
Yanga ilikamilisha maandalizi jana, Kocha Nasreddine Nabi akisema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa mgumu
US Monastir wamekuwa na msimu mzuri kwenye ligi ya Tunisia wakiwa vinara wa kundi B
Ni timu ambayo makazi yake yako kwenye mji wa Sousse, Mji ambao kocha Nabi ndiko alikozaliwa pia
Mchezo huo utapigwa katika jiji la Tunis katika uwanja uleule ambao Yanga waliwafunga Club Africain na kutinga makundi
Hivyo ni mchezo ambao Yanga inawania rekodi nyingine ya kuzifunga timu mbili za Tunisia kunako dimba la Hammadi Agrebi
Mashabiki na Wanachama wa Yanga jijini Dar es salaam ambao watapata nafasi ya kwenda Makao Makuu (Jangwani) kuhudhuria dua maalum ya kuiombea Yanga katika maadhimisho ya miaka 88, wataushuhudia mchezo huo kwenye TV KUBWA